Ole Gunnar Solskjaer aendelea kuwasha moto OT
Ole Gunnar Solskjaer ameendelea na kuwa na mwanzo mzuri tangu kutua Man United mwezi huu. Jana amefanikiwa kuondoka na ushindi wa tatu tangu aje Old Trafford, akishinda kwa goli 4-1 dhidi ya Bournemouth, mchezo wa ligi kuu nchini England.
Kiungo Paul Pogba ameendela kung’aa chini ya Solskjaer, ambapo jana alifanikiwa kufunga goli 2 na kutoa assist moja. Hii ni mechi ya pili mfululizo anafunga goli 2.
Magoli mengine ya Man United yalifungwa na Marcus Rashford na Romelu Lukaku ambaye alitokea benchi.
Ushindi huu unawafanya mashetani hao wekundu kufikisha pointi 35, wakiwa pointi tatu nyuma ya Arsenal ambao wapo katika nafasi ya tano.
Man United itashuka dimbani Januari 2 ambapo watakuwa ugenini St.James Park kucheza na Newcastle United