Mayweather aingiza bilioni 20 ndani ya dakika 2 Japan
Bondia kutoka nchini Marekani Floyd Mayweather,41, katika kuukaribisha mwaka mpya leo amejizolea kitita cha dola milioni 9 (Tsh Bilioni 20.6) ndani ya takribani dakika mbili tu baada ya kushinda pambano lake la dhidi ya Mjapan Tenshin Nasukawa huko nchini Japan.
Mayweather amemuangusha chini Nasukawa,21, mara tatu katika raundi ya kwanza kabla ya kona ya Nasukawa kurusha taulo kuashiria kukubali kushindwa.
Pambano hilo lililopigwa nje kidogo ya mji wa Tokyo, lilikuwa la raundi 3 na bila majaji, ushindi ulikuwa unaamuliwa na Knock Out au Technical Knouck Out.