Unai Emery apigwa faini na FA
Kocha wa Arsenal Unai Emery amepigwa faini ya pauni 8,000 ( Tsh milioni 23) na FA kwa kosa la kupiga chupa iliyoenda kumpiga shabiki katika mechi yao ya Disemba 26 dhidi ya Brighton iliyoisha kwa sare ya 1-1. Mhispania huyo aliomba msamaha kwa shabiki huyo baada ya mechi kumalizika na kutarajia tatizo hilo lingeishia hapo.