Shaqiri amwaga sifa kwa Bobby
Winga wa Liverpool Xherdan Shaqiri anaamini Hat Trick ya Roberto dhidi ya Arsenal jana itamfanya Mbrazil huyo kuimarisha zaidi kiwango chake.
Mbrazil huyo alikuwa amefunga goli 4 katika ligi kuu kabla ya mechi ya jana, na baada ya Hat Trick ya jana imemfanya kufikisha goli 7.
“ Alistahili (Hat Trick) kabisa. Alikuwa na mchezo mzuri “ Shaqiri alisema kupitia tovuti ya Liverpool.
“ Siku zote ni vizuri kuwa na watu wanaoweza kufunga katika timu, alifunga goli pili vizuri sana .
Alistahili kabisa kufunga Hat Trick na ninafuraha kwa ajili yake. Ninatumaini ataendelea kama hivi. “
Baada ya ushindi wa 5-1 jana, Liverpool imeendelea kuwa kileleni mwa ligi huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote. Alhamisi ya wiki ijayo watashuka dimbani kuwavaa Manchester City kwenye uwanja wa Etihad jijini Manchester.