LIGI YA MABINGWA IMEMRUDISHA ULIMWENGU NYUMBANI.
Baada ya shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF
kupanga makundi ya mashandano ya klabu Bingwa
Afrika kwa msimu wa 2018/19 na kujikuta
wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki Simba SC
wakiangukia Kundi D.
Inawezekana hufahamu kuwa hiyo itakuwa ni fursa
kwa mchezaji wa kitanzania kurudi kucheza
nyumbani akiwa na jezi ya klabu ya nje, Thomas
Ulimwengu toka ameanza maisha ya soka hajawahi
kucheza Ligi ya Tanzania hivyo wengi wanakuwa
wanakosa burudani yake uwanjani akiwa katika ngazi
ya vilabu.
Simba imepangwa Kundi D lenye timu za AS Vita Club
ya nchini Congo, Al Ahly ya nchini Misri na JS Saoura
ya nchini Algeria ikiwa ni siku chache tu imemsajili
mtanzania Thomas Ulimwengu aliyekuwa anacheza
Al hilal ya Sudan, hivyo kwa kuwa wamepangwa
Kundi moja ni wazi Ulimwengu atarudi kucheza
nyumbani dhidi ya Simba akiwa na JS Saoura hiyo
ikiwa ni mara ya pili kwa yeye kucheza uwanja wa
taifa akiwa na klabu baada ya kucheza dhidi ya Yanga
akiwa na TP Mazembe.