ROBINHO KUUNGANA NA EMMANUEL ADEBAYOR KWA MARA YA PILI
Mwanasoka wa zamani wa klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza Robinho ameripotiwa kuwa katika harakati za kukamilisha usajili wa kujiunga na wakali wa Ligi Kuu nchini Uturuki klabu ya Istanbul Basaksehir.
Robinho ambaye jina lake lilichukua vichwa vya habari vya kila kona katika magazeti ya michezo mwaka 2008 akitokea Real Madrid kwenda Manchester City alikodumu kwa miaka miwili kwa rekodi ya usajili ya pauni milioni 32.5 nchini Uingereza, muda wowote January anawezekana akajiunga na timu hiyo.
Kwa sasa Robinho anacheza Sivasspor ya nchini Uturuki pia, kama usajili wake ukikamilika mwezi Januari ataungana na mkali mwingine wa zamani wa Manchester City Emmanuel Adebayor ambaye anaichezea Istanbul Basaksehir pia, Robinho mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa ana mwaka mmoja toka arudi kucheza soka Ulaya.