Mbwana Samatta atengewa dau nono
Nyota wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji Mbwana Samatta ameripotiwa kuhitajika na klabu ya Ligi daraja la kwanza nchini England ya Middlesbrough, klabu hiyo imejipanga kutuma ofa nono kwa Genk mwezi Januari.
Middlesbrough ambayo kwa sasa ipo nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Daraja la kwanza maarufu kama Championship, imepanga kulipa ada ya usajili ya pauni kati ya milioni 7-8 sawa na Tsh Bilioni 23.3 ili kuishawishi KRC Genk imuachie mchezaji huyo mwezi Januari katika dirisha dogo.
Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa Mbwana Samatta kuripotiwa kuhitajika na vilabu mbalimbali barani Ulaya, ilianza kwa timu ya Fenerhbace ya Uturuki, baadae Everton, West Ham United, Brighton zote za Uingereza na Levante ya Hispania, licha ya mirror kuripoti staa huyo kuhitajika na Middlesbrough ila Samatta ameongeza kandarasi ya kuitumikia KRC Genk hadi mwaka 2021.