Serengeti Boys kuweka kambi Ulaya
Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa wenyeji wa michuano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17. Michuano hiyo itafanyika mwakani April 14-28.
Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia amesema timu yao ipo tayari kwa ajili ya michuano hiyo na mwakani itaweka kambi barani Ulaya kujiandaa na michuano hiyo.
Katika michuano hiyo Tanzania imepangwa kundi ikiwa na timu za Nigeria,Angola na Uganda, huku kundi B likiwa na timu za Guinea,Cameroon,Morocco na Senegal.
Timu nne ambazo zitaingia hatua ya nusu fainali kwenye michuano hiyo, zitakuwa zimefuzu kuingia katika fainali za kombe la Dunia.