Ole Gunnar Solskjaer kawatoa hofu wachezaji wa Man United “NATAKA WAFURAHIE SOKA”
Mwalimu wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kueleka mchezo wake wa kwanza ya Ligi Kuu ya nchini Uingereza dhidi ya Cardiff City ugenini,. Ole Gunnar Solskjaer amsema lengo lake ni kutaka kumfanya kila mchezaji awe na furaha na morali ya kucheza soka kama ambavyo baadhi ya watu wanaipata wakiwa na timu zao.
“Ninachotaka kufanya ni kuhakikisha wachezaji wanafurahia soka tunacheza kwa ajili ya mashabiki wetu na fahari yetu kuichezea hii klabu ni historia ya kipekee nalazimika kusema hivyo, naijua hii klabu na naielewa historia yah ii klabu, utamaduni wake imekuwa ikiwa wapa nafasi nyota wadogo ya kucheza na kushinda mataji, huwezi kuamini namna ilivyoniendeleza tokea nimekuja hapa mwaka 1996” alisema Ole Gunnar Solskjaer ambaye ni kocha wa muda wa Manchester United.
Ole Gunnar Solskjaer anakuwa na wakati wa kuhakikisha anainusuru Manchester United na kuifanya irudi katika nafasi nne za juu baada ya kuwa na mwanzo mbaya wa msimu na imekuwa timuya kupigwapigwa tu, kwa sasa ipo nafasi ya 6 kwa kuwa na alama 26 ikicheza michezo 17 hivyo inapambania walau kumalinza nafasi za juu na kukata tiketi ya kucheza klabu Bingwa Ulaya msimu ujao,.