AUSSEMS KAELEZA UKWELI HANA TIME NA KMC, ANAWAFIKIRIA NKANA FC TU !!
Kocha mkuu wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Patrick Aussems ameweka wazi baada ya kurejea nchini kuwa jicho na akili yake lipo katika mchezo wa marudiano na Nkana Red Devils Jumapili ya Desemba 23 lakini sio mchezo wa Jumatano hii ya Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya KMC.
Aussems ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo dhidi ya KMC akiwa na viporo vinne vya Ligi Kuu atacheza akiwatumia wachezaji ambao hawapati nafasi zaidi ili kuwapumzisha wachezaji wake kwa mchezo alioupa nguvu zaidi wa siku ya Jumapili wa Klabu Bingwa Afrika 2018/2019 dhidi ya Nkana FC ya Zambia.
“Kuwa mkweli kwenu tunaangalia mchezo wa Klabu Bingwa Afrika zaidi kuhusu KMC tuna taarifa zao baadhi husuani wasaidizi wangu tunajua kuwa walishinda tano mchezo uliopita lakini tutabadilisha kikosi kuelekea mchezo huo huwezi kuwatumia wachezaji walewale tu, kama nilivyowaambia wiki za nyuma nina waamini wachezaji wangu wote na mchezao dhidi ya KMC nitawatumia wachezaji wangu ambao hawakucheza maraya mwisho” alisema Patrick Aussems baada ya kutua Dar es salaam wakitokea NdolaZambia.
Simba SC wanakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC ya Kinondoni inayofundishwa na kocha Ettiene Ndairagije lakini pia ina mtihani wa kuwania tiketi ya kuendelea hatua inayofuata ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia siku ya Jumapili kufuatia mchezo wa kwanza kupoteza kwa mabao 2-1, hivyo watalazimika kusaka ushindi wa bao 1-0 au ushindi wa kuanzia mabao 3-1, Ligi Kuu Simba wana viporo vinne wakiwa wamecheza michezo 12 na wapo nafasi ya tatu wakizidiwa michezo minne ya Yanga na Azam FC waliopo juu yao katika msimamo wa Ligi Kuu.