Majogoo wamuadhibu Mourinho Anfield
Majogoo wa jiji wamerudi kileleni mwa ligi baada ya kuibuka na ushindi katika uwanja wao wa nyumbani Anfield dhidi ya wapinzani wao wakubwa Manchester United.
Sadio Mane ndio alikuwa wa kwanza kuziona nyavu dakika ya 24 kabla ya Jesse Lingard kutumia makosa ya kipa wa Liverpool Allison Becker kusawazisha katika dakika ya 33 ya mchezo.
Mabadiliko ya Jurgen Klopp ya kumtoa Naby Keita na kumuingiza Xherdan Shaqiri dakika ya 70 yalizaa matunda katika dakika ya 73 baada ya Shaqiri kuipa Liverpool goli la uongozi kabla ya kuongeza lingine kunako dakika ya 80 na kuhakikisha ushindi kwa majogoo.
Mchezo uliisha kwa Liverpool kushinda 3-1. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Liverpool katika ligi dhidi ya Man United kwenye uwanja wa Anfield tangu mwaka 2013.
Liverpool wanarudi kwenye usukani wa ligi wakiwa na pointi 45, City wakishika nafasi ya pili na pointi 44 huku vijana wa Jose Mourinho wakiwa nafasi ya sita na pointi 26.