THOMAS MULLER AOMBA RADHI KWA NICO WA AJAX
Mshambuliaji wa Bayern Munich ya nchini Ujerumani Thomas Muller ameamua kuomba msamaha hadharani kufuatia kitendo chake cha kumchezea faulo ya hatari mchezaji wa Ajax Nico Tagliafico katika mchezo dhidi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano.
Mechi hiyo ilimalizika kwa Muller kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 75 kufuatia kitendo cha kumchezea faulo ya hatatri Nico Tagliafico katika sare ya kufungana mabao3-3 ila wote Bayern na Ajax wamefuzu kucheza hatua inayofuata ya 16 bora yaLigi ya Mabingwa Ulaya.
Muller ameamua kuomba radhi Nico Tagliafico na kumtakia kheri apone haraka mchezaji huyo“Ningependa kumuomba radhi Nico Tagliafico kwa tukio lililotokea jana, kilikilikuwa ni kitendo ambacho sio cha kukusudia nakutakia upone haraka” alisemaThomas Muller
FC Bayern Munich wameingia hatua ya 16 bora kwa kuongoza Kundi j
Kwa alama 14 wakishinda mechi 4 sare mechi 2, wakifuatiwa na Ajax kwa kuwa na alama 12,washinda mechi 3 na sare mechi tatu, wote Bayern na Ajax hawajapoteza mchezo.