MKURUGENZI WA BARCELONA WA ZAMANI ANASEMA NI UAMUZI WA HATARI KUMSAJILI DEMBELE
Hivi karibuni ilielezwa kuwa klabu ya Barcelona imemuita wakala wa mchezaji wao Ousmane Dembele na kukaa nae kujadiliana kuhusiana na tabia ya mchezaji huyo ya kuwa mchelewaji sugu wa mazoezi ya timu licha ya kupigwa faini, Dembele Jumapili iliyopita alichelewa kwa saa 2 katika mazoezi ya Barcelona ya kujiandaa dhidi ya Espanyol.
Dembele amepigwa faini ya zaidi ya euro 50000 toka amejiunga na FC Barcelona miezi 18 iliyopitana faini zote hizo ni kutokana na tabia yake ya uchelewaji, kufuatia taarifa hizo mkurugenzi wa michezo wa zamani wa Barcelona Urban Ortega amesema kuwa ilikuwa ni uamuzi wa hatari kuamua kumsajili Dembele kutokana na tabia zake
“Tayari tulikuwatunajua kuhusiana na yeye (Dembele) kiukweli alikuwa tayari na matatizo alipokuwa Rennes ambapo alikuwa hataki kusaini mkataba wa kucheza professional, tayari tulikuwa na taarifa za matatizo yake kiufundi na baadhi ya taarifa kuhusu utovu wa nidhamu kutokana na ujana wake na watu wanaomzunguuka lakini tuliamua maamuzi ya hatari ya kumsajili yeye badala ya Mbappe”alisema Ortega
Ortega akishirikiana na Roberto Fernandez alikuwa sehemu ya watu waliofanya uhamishowa Dembele kutokana Dortmund kujiunga na Barcelona utimie mwaka 2017 la ada ya uhamisho inayotajwa kufikia euro milioni 105, Dembele alifunga mabao manne msimu uliopita akiichezea Barcelona katika mechi 23 lakini ameonesha kuimarika msimu huu baada ya kufunga mabao nane katika mechi 17