EMMANUEL MARTIN AMEONDOKA YANGA
Mabadiliko ya makocha ni kitu ambacho kimekuwa kikiwaathiri wachezaji wengi wa soka, hii inatokana na utamaduni au taratibu za makocha wapya kuingia katika timu mpya wakiwa na mbinu na falsafa zao mpya kitu ambacho kinakuwa pigo kwa baadhi ya wachezaji.
Janga hilo limemkuta mshambauliaji wa Yanga Emmanuel Martin ambaye amelazimika kujinga na klabu ya Ruvu Shooting baada ya kutopata nafasi katika kikosi cha Yanga toka awasili kocha raia wa Congo Mwinyi Zahera ambaye imeonekana kama Martin hayupo katika mipango yake.
Emmanuel Martin ambaye ameondoka Yanga na kujiunga na Ruvu Shooting baada ya mkataba wake kumalizika na kutopewa mkataba mpya, alijiunga na Yanga miaka miwili iliyopita akitokea klabu ya JKU ya Zanzibar, akiwa Yanga amewahi kuitwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Emmanuel Martin anaingia katika vitabu vya kumbukumbu vya muhispani Juan Mata ambaye alikumbana na dhahama kama ya kwake baaada ya Jose Mourinho kujiunga na Chelsea alimtoa mchezaji huyo kwenye mipango yake na kujikuta anauzwa kwenda Manchester United kinyume na matarajio ya wengi.