TIMU ZILIZOINGIA 16 BORA NA WALIOANGUKIA EUROPA LEAGUE
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi msimu wa 2018/19 imemalizika kwa usiku wa Jumatano wa Desemba 12 2018 kuchezwa michezo nane iliyohitimisha hatua hiyo, hivyo sasa tumejua timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora na timu zilizofanikiwa kuangukia michuano ya Europa League.
Mechi nyingi zilizochezwa usiku wa Desemba 12 zilikuwa za kukamilisha ratiba na baadhi yatimu zilikuwa zinajua kuwa zimeshafanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya michuano hiyo msimu wa 2018/19, timu za Inter Milan, Club Brugge, Napoli, Valencia, Pizen, Benfica, Shakhtar na Galatasaray ndio zimeangukia Europa League.
Timu za Ajax, Atletico Madrid, FC Barcelona, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Juventus, Liverpool, Olympique Lyon, Man City, Man United, PSG, Real Madrid, Roma, Tottenham, Schalke 04 na FC Porto ndio zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ukaya.