REAL MADRID WAMESEMA INAWEZEKANA RONALDO ANA JAMBO LA SIRI KUSEMA JUVENTUS NI FAMILIA YAKE
Klabu ya Real Madrid imekuwa ikiyumba kupata matokeo chanya toka ameondoka nyota wao wa zamani Cristiano Ronaldo na kujiunga na timu ya Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 105 katika kipindi cha usajili cha majira ya joto.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 wiki hii alitoa kauli nzito kwa vyombo vya habari ikiwemo ndani ya muda mfupi tu akiichezea Juventus, amesema anajisikia kuwa yupo kama nyumbani ila Real Madrid wamesema Ronaldo anaweza kuwa anasababu iliyojificha ya kusema Juventus ni familia yake.
“Wachezaji Juve ni wanyenyekevu na wanacheza kwa ushirikiano, Juve ni timu nzuri kuwahi kuichezea katika maisha yangu ukilinganisha na baadhi ya timu ambapo kuna wachezaji wanajihisi wao ni bora kuliko wenzao, hapa kila mmoja mnyenyekevu Dybala na Mandzukic wanaweza wasifunge lakini bado wakawa na furaha” alisema Cristiano Ronaldo
Watu wa Real Madrid ikiwemo stafu wa Real Madrid wanadaiwa kuichukulia poa kauli hiyo na kusema inawezekana Ronaldo aliitoa hili kuwateka mashabiki wa Juventus kuzidi kupenda na hakuna ukweli wowote, hiyo ni kwa mujibu wa Ok Diario.