REAL MADRID WAMEMNASA KINDA WA RIVER PLATE
Mabingwawatetezi wa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya Real Madrid wanahusishwa kuwa wamemalizana na kiungo wa timu ya River Plate ya Argentina Exequiel Palacios, Real Madrid wanatajwa kuwa watambambulisha mapema mwezi huu mara baada ya klabu Bingwa Dunia.
Exequiel Palacios ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha River Plate kilichocheza katika uwanja wa Santiago Bernabeu dhidi ya Boca Junior katika mchezo wa fainali yapili wa Kombe la Lebaratoe uliyomalizika kwa River Plate kupata ushindi wa 3-1.
Kiungo huyo wa River Plate Exequiel Palacios alidaiwa kuwindwa kwa zaidi ya miezi kadhaa na sasa atakuwa mali ya Real Madrid baada ya fainali za michuano yaKombe la dunia ngazi ya vilabu Desemba 22 ambapo wao River Plate na Real Madridwataanzia hatua ya nusu fainali.