Boban rasmi mali ya Yanga
Mchezaji mkongwe Haruna Moshi Bobani leo rasmi amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kukitumikia kikosi cha Yanga
Akizungumzia usajili huo kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alisema kuwa alivutiwa na Boban baada ya kumuona kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya African Lyon dhidi ya JKT Tanzania
Tukukumbushe kuwa Haruna Moshi Boban anayetajwa kuwa miongoni mwa viungo bora kuwahi kutokea nchini amewahi kucheza soka katika timu mbalimbali ndani ya Tanzania na nje yaTanzania, Boban ameichezea Moro United (2003-2004), Simba SC (2004-2009), GefleIF ya Sweden (2010-2011) na Mbeya City pia.