HAZARD AMETANGAZA KUUNGANA NA RAHEEM STERLING WA MANCHESTER CITY
Ikiwa ni siku chache zimepita toka Polisi jijini London watangaze kuanza uchunguzu wa kitendo kilichotokea katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza kati ya Manchester City dhidi ya Chelsea jijini London katika uwanja wa Stamford Bridge.
Mechi hiyo ambayo ilichezwa na kushuhudiwa Manchester City wakivunja rekodi yao ya kucheza michezo 20 ya Ligi Kuu Uingereza pasipo kupoteza walifungwa mabao 2-0, Chelsea wakiwa nyumbani lakini kuna kitendo cha ubaguzi wa rangi kilifanywa na mashabiki wa Chelsea kwa Raheem Sterling wa Manchester City.
Raheem wakati mchezo huo ukiendelea akienda sehemu karibia na mashabiki wa Chelsea kuokota mpira ili apige kona, alitolewa maneno ya kuashiria ubaguzi wa rangi na mashabiki wa Chelsea dhidi yake, nyota wa Chelsea Eden Hazard ameoneshwa kusikitishwa kwake kwa kitendo alichofanyiwa.
“Kuna uchunguzi unaendelea hivyo hatujui nini kitatokea, mashabiki sahihi wa Chelsea ni wale wanaoiimbia Chelsea na kufurahia mechi, naungana na Raheem kupinga hiki kitendo cha ubaguzi wa rangi na hakika hakitaendelea kuwepo uwanjani tena” alisema Eden Hazard