Gor Mahia yamteua Oktay
Mwabingwa wa Kenya, Gor Mahia wamemteua raia wa Uturuki, Hassan Oktay kama kocha wao mpya.
Oktay anajiunga na Gor Mahia kwa kandarasi ya miaka miwili na atakuwa na jukumu la kubadili matokeo ya timu ya Gor Mahia ambayo kwa sasa si mazuri.
Gor Mahia imepoteza mechi tatu kwa mpigo na mechi yao dhidi ya Zoo siku ya Jumatano itawapa nafasi ya kujikwamua.
“Tumemteua Hassan kama mridhi wa Dylan Kerr, ametia wino kwenye kandarasi ya miaka miwili. Zedekiah Otieno atakuwa msaidizi wake. Endapo ataridhisha, tutamwongeza kandarasi,” alisema mwenyekiti wa Gor Mahia, Ambrose Rachier.
Gor ilichapwa na Bandari kwenye mechi yao ya kwanza siku ya Jumamosi.