Tusker yamsajili ‘Adebayor’
Timu ya Tusker FC imemsajili mshambulizi wa timu ya Gor Mahia Kevin ‘Adebayor’ Omondi kwa kandarasi ya miaka miwili.
Omondi ambaye alirejea kwenye timu ya Gor mwanzo wa mwaka huu ameruhusiwa kuwakacha ligi ya Kenya baada ya kutowaridhisha wakufunzi wa Gor.
Akizungumza baada ya kusajiliwa, Ade alisema huko tayari kupigania nafasi yake kwenye timu hiyo.
“Nina furaha kujiunga na klabu ya Tusker. Tusker ni timu yenye wachezaji wazuri na niko tayari kupigania nafasi yangu kwenye timu,” alisema mshambulizi huyo ambaye ashawahi ichezea timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.
Ade ashawahi ichezea vilabu vya Sofapaka, Kariobangi Sharks, Nakumatt na Kenya Police FC.
Wachezaji wengine wapya kwenye timu ya Tusker in pamoja na Muzerwa Amani, Emery Mvuyekure, Mike Madoya, Nashon Alembi, Clyde Senaji, Sammy Meja, Hillary Wandera, Rogers Aloro na Bill Oporia.