INTER WAMESHINDWA KUIZUIA JUVENTUS TURIN
Ligi Kuu Italia usiku wa Desemba 7 2018 ulitekwa na mchezo mmoja wa tu wa Serie A kati ya klabu ya Juventus dhidi ya klabu ya Inter Milan, Juventus ambao wanaongoza Ligi wakiwa hawajapoteza mchezo zilianza kuzuka tetesi kuwa wanaweza wakapoteza mchezo huo kutokana na Inter Milan kumiliki mpira.
Licha ya hali ya umiliki wa mpira hadi dakika 90 zinamalizika zilikuwa ni asilimia 51 kwa Inter Milan na Juventus asilimia 49, hali ya mchezo haikuwasaidia na Mario Mandzukic akafunga bao pekee la Juventus dakika ya 66 na kuufanya mchezo umalizika kwa bao 1-0, hivyo alama tatu muhimu zimebaki Turin.
Juventus hadi sasa wanaendeleza rekodi ya kuwa timu pekee Serie A ambayo haijapoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu ikicheza michezo 15, ikishinda michezo 14 na kusuluhu mchezo mmoja pekee, Juventus sasa mchezo ujao watakuwa wanacheza dhidi ya Torino Desemba 15 2015 ugenini katika uwanja wa Stadio Olimpico.