Joe Gomez wa Liverpool tunasubiri ripoti ya daktari
Beki wa Liverpool Joe Gomez ameshindwa kumaliza mchezo wa Ligi Kuu Uingereza kati ya timu yake ya Liverpool dhidi ya Burnley na kujikuta akitolewa nje ya uwanja kutokana na kupata majeraha ya kifundo cha mguuu.
Mchezo huo uliochezwa ugenini na Liverpool kupata ushindi wa mabao 3-1, Joe Gomez alifanikiwa kucheza kwa dakika 23 pekee na kutolewa nje ya uwanja baada ya kuchezewa vibaya na Ben Mee na nafasi yake kuchukuliwa na Alexander Arnold.
Kwa sasa ripoti ya daktari ndio inasubiriwa kujua hali ya Gomez, pamoja nah ayo ushindi huo umeisaidia Liverpool kuendelea kusalia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwani wamefikisha jumla ya alama 39 wakicheza michezo 15, wakishinda michezo 12, sare michezo 3 na hakuna mchezo waliopoteza.