MANCHESTER CITY TENA BILA AGUERO MOTO NI ULE ULE TU!!!
Bado Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza Manchester City wanaendelea kukosa huduma ya mfungaji wao bora wa muda wote wa klabu hiyo Sergio Aguero kwa kuwa anaendelea kuuguza majeraha yake hivyo Guardiola amemuacha awe fiti ndio aanze kumtumia.
Kocha Pep Guardiola akimkosa Aguero amekiongoza kikosi chake mchezo wao dhidi ya Watford wakiwa ugenini katika uwanja wa na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1, mabao hayo yakitiwa wavuni na Leloy Sane dakika ya 40 na Riyad Mahrez dakika ya 51 wakati bao la Watford limefungwa na Abdoulaye Doucourse dakika ya 85.
Manchester City sasa wanapata ushindi wa 13 wakicheza michezo yao 15 ya Ligi Kuu Uingereza sare ikiwa michezo miwili na hawajapoteza mchezo hata mmoja msimu huu sawa na Liverpool waliopo nafasi ya pili kwa kuwa na alama 36 ila Manchester City wakiongoza kwa kuwa na alama 41.