PATRICK AUSSEMS ATAJA MBINU WALIOITUMIA SIMBA KULAINISHA UKUTA WA MBABANE SWALLOWS
Kocha mkuu wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC Patrick Aussems aliamua kuweka wazi mbinu aliyoitumia ili kulainisha ukuta wa ulinzi wa Mbabane Swallows katika mchezo wa kwanza wa mzunguuko wa kwanza wa klabu Bingwa Afrika.
Patrick Aussems ameeleza baada ya ushindi wa mabao 4-1 uwanja wa Taifa katika mchezo dhidi ya Mbabane ni kuwa, waliwahi kujua mapema kuwa wapinzania wao ni timu imara zaidi ila alichokiona kinachoweza kuubomoa ukuta wa Mbabane na kupata matokeo ni kuwapa presha kwa kushambulia kwa kasi kitu ambacho kilizaaa matunda.
“Tunajua tulikuwa tunacheza dhidi ya mpinzania mzuri na ndio maana tuliamua toka mwanzo wa mchezo kuwapa presha, tulianza vizuri uliona tulipata goli la kwanza kabla ya dakika ya nane au ya tisa, kwa bahati mbaya baada ya dakika ya 20 walipiga shuti moja lililolenga lango la kufunga goli lakini nimeridhishwa na uwezo wa wachezaji wangu na hawakukata tamaa na kuendelea kucheza kwa kupambana” alisema Patrick Aussems
Tukukumbushe tu baada ya matokeo hayo Simba SC watalazimika kwenda Mbabane nchini Swaziland kucheza mchezo wa marudiano huku wakiwa wanahitaji sare ya aina yoyote au afungwe chini ya goli 3 katika mchezo wa Marudiano Decemba 4 au 5, 2018.