Simba SC kuwakosa Kwasi, Kapombe na Juuko kesho
Afisa habari wa klabu ya wekundu wa Msimbazi SimbaSC, Haji Manara jana Novemba 26 kwenye mkutano nawaandishi wa habari alitangaza kuwa wachezaji wao wakimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi na JuukoMurshid wangewasili mapema ila imekuwa tofauti.
Kuelekea mchezo wao wa mzunguuko wa kwanza wamichuano ya klabu Bingwa Afrika, Simba SC kupitiakwa kocha wao wa makipa Mwalami Mohamed aliongeana waandishi wa habari na kutoa taarifa kuwa timu yaoipo kamili ila wamkosa Shomari Kapombe aliyepoAfrika Kusini na Juuko Murshid ana matatizo yakifamilia.
“Tuna matatizo kidogo tuna majeruhi ya mchezaji wetuKapombe na Asante Kwasi lakini na Juuko ambayeameshindwa kurejea kutoka Uganda alipokuwaanaitumikia timu ya taifa kutokana na matatizo yakifamilia, tunaomba watanzania wote watuunge mkonokesho sisi tunaiwakilisha nchi” alisema MwalamiMohamed
Simba SC kesho itacheza mchezo wake wa kwanza wamzunguuko wa kwanza hatua ya mtoano uwanja waTaifa dhidi ya Mbabane Swallows kabla ya kurudiananchini Swaziland siku zijazo.