Jose Mourinho awabwatukia wachezaji wake
Leo Jumanne ya mwezi Novemba 27, 2018 Manchester United watacheza mchezo wao wa Kundi H wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wageni wao Young Boys ukiwa huo ni muendelezo wa michezo ya hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/2019.
Manchester United watakuwa nyumbani lakini maneno yameanza na hofu kwa baadhi ya mashabiki kuwa inawezekana wasifanye vizuri au wachezaji wao wasicheze kwa kiwango cha juu ukilinganisha na michezo ya ugenini kutokana na presha ya mashabiki katika uwanja huo.
Kuelekea mchezo huo kocha wa Mnanchester United Jose Mourinho amefunguka na kueleza kuwa kama wachezaji wake wabaki manyumbani kwao na kuangalia mechi ya Man United kwa runinga kama wanashindwa kukabiliana na presha ya kucheza uwanja wa nyumbani
“Kama una presha kucheza Old Trafford baki nyumbani utazame mechi kwenye TV, kuna mashabiki watakuja kutusapoti waje m, sijisikii presha kucheza katika uwanja wa nyumbani, itakuwa ni kuwakosea heshima mashabiki wetu kwa kusema kuwa tunapendelea kucheza ugenini zaidi kuliko nyumbani” alisema Jose Mourinho
Manchester United ambayo itacheza mchezo wake wa tano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Young Boys kwa sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na alama saba, alama mbili nyuma ya Juventus wanaoongoza kwa kuwa na alama 9, Manchester United msimu huu wakiwa Old Trafford wamecheza michezo 9 na kupata ushindi michezo mitatu, hivyo rekodi hazipo upande wao upande wa uwanja wao wa Old Trafford.