Mtibwa Sugar waanza kwa kishindo michuano ya kimataifa
Kikosi cha Mtibwa Sugar kimefanikiwa kuanza vizuri michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kushinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Northern Dynamo ya Shelisheli mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Mchezo huo umeweka rekodi mpya kwa Mtibwa ya kufunga ‘Hat-trick’ ya Jaffary Kibaya ambaye amefanikiwa kutumia nafasi ambazo walizitengeneza Mtibwa leo. …