Hatimaye Thierry Henry aonja raha ya ushindi
Thierry Henry amefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza akiwa kocha wa Monaco hapo jana timu yake ikiibuka kidedea kwa kushinda goli 1-0 dhidi ya Caen ugenini kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Ufaransa.
Ushindi huu umekuja katika mechi yake ya saba kwenye timu hiyo ambayo alijiunga nayo mwezi Oktoba mwaka huu akichukua nafasi ya Leonard Jardim.
Goli zuri la Free-kick likifungwa na Radamel Falcao dakika ya 54
ndio limempa ushindi Henry ambaye amefanya kazi na timu kwa takribani wiki sita sasa.
Mabingwa hao wa 2017 walikuwa hawajashinda mechi yoyote tangu Agosti 11 mwaka huu, na ushindi huu wa pili katika ligi msimu huu.
Nafasi ya 19 ndio wanashika katika msimamo wa ligi wakiwa na jumla ya pointi 10.
Kabla ya ushindi wa jana, Henry amepata sare mbili na kufungwa mechi nne akiwa kocha timu hiyo, na ushindi huu dhidi ya Caen unafufua matumaini na kumpunguzia Pressure baada ya kuwa na mwanzo mbaya katika timu hiyo.