Gari ya Steph Curry yapata ajali
Gari la Staa wa Warriors Steph Curry lilikuwa mojawapo ya magari matatu yaliyogongana huko Oakland , California Marekani jana Novemba 23 saa tatu asubuhi kwa saa za Marekani
Imeelezwa kuwa gari la Steph Curry, aina ya Porsche liligongongwa mara mbili na kuharibiwa, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyeumia katika ajali hiyo.
Steph Curry bado anauguza majeraha yake na leo amekosa mechi nyinngine ya Warriors ambayo walicheza na Blazers na kushinda kwa pointi 125-97.