RUMORS ZA USAJILI
Chelsea inaungana na Manchester United kumfatilia mlinzi wa Inter Milan Milan Skriniar mwenye thamani ya pauni 70.(sun)
Manchester United inatazamia kumsajili beki wa Fiorentina na Serbia Nikola Milenkovic,21, katika dirisha la usajili mwezi Januari (Sky Sports)
Winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 20 Christian Pulisic ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na Liverpool anaamini kuwa Jurgen Klopp ni aina ya meneja wa wachezaji wote wa ndoto ya kufundishwa nae. (Liverpool Echo)
Beki wa Kati wa Manchester City Mfaransa Aymeric Laporte amesema itabidi afikie uwezo wa Sergio Ramos wa Real Madrid ili kutajwa kuwa beki bora duniani (Evening Standard)
Didier Drogba anaamini meneja wake wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho angeweza kushinda mataji “mara mbili au tatu” kama angekuwa anaiongoza Manchester city na sio majirani zao Manchester United (Mirror)
Barcelona inataka Mshambuliaji wa Brazil Neymar, mwenye umri wa miaka ,26, kuchukua hatua ya kumaliza muda wake huko Paris St-Germain, na kulazimisha kurejea Camp Nou. (Goal)
Mchezaji wa zamani wa Barcelona na Spain Xavi Hernandez anayecheza klabu ya Al Sadd huko nchi Qatar- anaamini Pep Guardiola ataibadili Man City kwenda kuwa klabu bora barani Ulaya. ( Express)
Meneja wa Man City Pep Guardiola anahisi atakwenda katika kufundisha timu za Taifa hivi karibuni au baadae ( Telegraph )