Virgil Van Dijk aonesha ushujaa uwanjani
Nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi Virgil Van Dijk alitumia muda wake baada ya mechi yao dhidi ya German kumfariji muamuzi aliochezesha mechi hiyo jumatatu Ovidiu Hategan kufuatia kupoteza mama yake mzazi.
Beki huyu wa kati wa Liverpool alifunga katika dakika ya 90 kwenye uwanja wa Gelsenkirche na matokeo kuwa 2-2 yakahakikisha timu yake inafuzu nusu fainali ya Uefa Nations League baada ya Kundi la 1 la League A.
Baada ya kushangilia kufuzu akiwa na timu yake , Van Dijk alikwenda kuzungumza na Hategan Mwenye asili ya Kiromania, ambaye alionekana akiangusha machozi, alimkumbatia na kutoa maneno ya kumfariji kufuatia msiba huo.
Van Dijk aliiambia Fox Sports baada ya mechi kuwa “ Refa alipoteza mama yake , niliona akivuja machozi machoni pake. Nilimwambia aendelee kuwa na nguvu na kwamba alichezesha mechi vizuri.
Ni kitu kidogo, lakini ninadhani itasaidia. “
Uholanzi ambayo ilishindwa kufuzu Kombe la mataifa ya ulaya 2016 na Kombe la Dunia la nchini Urusi, wamefurahia mabadiliko makubwa katika timu yao chini ya Ronald Koeman.