Rais wa klabu Napolia Aurelio De Laurentis kununua klabu Uiengereza.
Akiwa ametoka kamilisha ununuzi wa klabu ya Bari inayoshiriki Serie D na kumuachia mtoto wake wa kiume Luigi kuisimamia kama Rais, sasa Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentis amesema yupo sokoni kutafuta klabu ya England.
Haya yamekuja baada ya mzozo unaoendelea juu ya uwanja wa Stadio San Paolo usiomridhisha rais huyu.
Uwanja huu unaomilikiwa na jiji la Napoli unatumika na timu yake kwa makubaliano ya kulipa kodi ha Yuro Millioni 1.8 kwa mwaka.
Amelalamika na kusema kama hatouziwa uwanja huo atajenga uwanja mwingine sehemu nyingine na kuihamisha klabu hiyo.
Kumekuwa na mgongano juu ya marekebisho na matengenezo ya uwanja huo ambao umepelekea klabu hiyo kuchelewa uza tiketi zake kutokana na kuchelewa kwa uwekaji wa siti mpya katika uwanja huo. Zoezi hili linatakiwa fanyika majira ya joto ila hadi sasa hakuna maandalizi yeyote yaliyoanza fanyika.
Hili ni mara ya pili anatishia kuihamisha klabu katika uwanja huo baada ya hapo nwezi wa tisa kutishia kuhamisha mechi zote za Klabu Bingwa katika uwanja wa Klabu ya Bari uliopo kilomita 264 kutoka uwanja wa Napoli. Huku akisema atakodi mabasi 1,000 ya kuwabeba mashabiki kwenda na kurudi.
“Jambo la aibu sana. Nasema imetosha sasa. Sitaki husika tena na mambo haya. Nitajenga uwanja wangu. Hatuwezi kwenda hivi.”
Akiongea na ESPN nchini Italia amesema ahisi kama ataipeleka mbali Napoli kwa hivi vikwazo anavyovipata anapotaka kuuboresha.
Uwanja huo haujafanyiwa marekebisho yeyote makubwa tokea Kombe la Dunia mwaka 1990.
“Usimamizi wa uwanja ule ni tatizo. Jiji halijafanya chochote zaidi ya kuufanyia biashara tu.”
“Nilipogundua PSG wanalipa Yuro Millioni 1 Parc des Princes, niligundua vile tulivyo nyuma.”
“Wapo na siti 47,000. Wanatengeneza Yuro Millioni 100 kwa mwaka huku sisi tunatengenza Yuro millioni 17 mpaka 18 San Paolo. Hatuwezi fanya shughuli nyingine yeyote ya ziada.”
“Jiji halifanyi lolote juu ya San Paolo tolea mwaka 1990. Hakuna anayewajibika na majukumu hivyo tumejikuta na uwanja sio tu mbaya bali unaoelekea kuwa gofu. Kunayesha hadi ndani sasa.”
“Ingekuwa ni kwa amri yangu ningenunua ardhi ndani ya sekunde mbili na kujenga uwanja mpya ila kupo na mambo mengi ya kuzingatia.”
“Tumefeli kufanikisha fura zote za miaka ya hivi karibuni. Eneo la maduka halifanyi kazi na hata sinema pia. Sijui namna ya kuufanya uwanja ukatupa faida siku zote saba za wiki, labda tutoe ofa ya kareoke.”