Timu nne za nusu fainali Uefa Nations League zatimia
Timu nne zimepatikana ambazo zitaenda kucheza hatua ya fainali ya michuano ya UEFA Nations League mwezi Juni 2019.
Uholanzi wamefika hatua hiyo baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Ujerumani na kufikisha pointi 7 katika kundi 1 kwenye League A.
Kundi 2 limeongozwa na Switzerland wakiipiku Belgium, kundi la 3 limeongozwa na mabingwa wa Ulaya Ureno ambao wamefuzu hatua ya nusu fainali bila ya nyota wao Cristiano Ronaldo.
Timu ya Taifa ya England ndio iliongoza kundi 4 baada ya mechi ya mwisho kushinda dhidi ya Croatia kwenye uwanja wa Wembley.
Timu zote ambozo zimeshika nafasi za mwisho katika makundi ya League A zimeshuka kwenda League B.