Kloop kuweka rekodi mpya Liverpool
Msimu 2007/8 Rafael Benitez aliiongoza Liverpool kucheza michezo 15 ya mwazo bila kupoteza na kuweka rekodi mpya dhidi ya ile ya mechi 13 iliyowekwa msimu wa 1990/91.
Wakiwa wamecheza michezo 12 (W9, D3) na kujikusanyia points 30, Liverpool wapo nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi Manchester City.
Weekend hii watasafiri kuwafuata Watford ambapo Kloop atahitaji ushidndi ili kufikisha points 33 katika michezo 13 ambayo itakuwa ni rekodi ya points nyingi kukusanya na timu hiyo katika michezo 13 ya mwanzo katika ligi mbele ya ile ya Rafael Benitez msimu 2008/9 alipojikusanyia points 32 katika michezo 13.
Ni klabu ya Arsenal ndio inashikilia rekodi ya kucheza msimu mzima bila kupoteza mechi (michezo 38). Rekodi inayoonekana ngumu kuvunjwa huku klabu za Manchester City, Liverpo na Chelsea zikiendelea na mbio zao za ubingwa katika hali ya kujaribu fikia rekodi hiyo.