Jose Mourinho atua tena kwa Diego Simeone
Man United walishindwa kumsajili beki wa Atletico Madrid katika dirisha la usajili lililopita, lakini hawajakata tamaa ya kumleta Mruguay huyo Old Trafford
Atletico Madrid wameripotiwa kuwa wapo katika mazungumzo ya kumpa mkataba mpya beki huyo na Man United wanafuatilia kwa ukaribu majadiliano hayo
Godin na wawakilishi wake walikataa ofa ya Pauni milioni 20 kutoka kwa mashetani wekundu licha ya mazungumzo ya mkataba mpya na Atletico kutofikia makubaliano.
United wanataka kumsajili beki huyo,32, kwa ada ya kawaida kwa sababu ya umri wake lakini mchezaji huyo bado anatajwa kuwa moja ya walinzi bora duniani kwa sasa.
Pia Jose Mourinho anataka kumchukua kwa mkopo beki wa kati wa Chelsea Gary Cahill katika dirisha la mwezi Januari kutokana mchezaji huyo kutokuwa na furaha kwa kukosa nafasi ya kikosi cha kwanza kwa Maurizio Sarri.