Santiago Solari kocha Mkuu Real Madrid hadi 2021
Nchini Hispania klabu hairuhusiwi kuwa na kocha wa muda ‘ Caretaker’ kwa zaidi ya wiki mbili.
Santiago Solari ametangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Real Madrid mpaka mwaka 2021.
Mkataba huo umekuja baada ya Muargentina kuiongoza Real Madrid kushinda mechi zote nne tangu apewa timu kama kocha wa muda kufuatia Julen Lopetegui kutimuliwa.