Draymond Green akosa mechi baada ya kugombana na Kevin Durant
Draymond Green amekosa mechi ya leo ya timu yake ya Warriors dhidi ya Atlanta Hawks kufuatia kufungiwa na uongozi wa timu hiyo kwa kosa alilofanya kwenye mchezo wa jana waliopoteza dhidi ya LA Clippers.
Green aligombana na mchezaji mwenzake wa Warriors Kevin Durant katika mchezo huo, ugomvi huo ulitokea baada ya Green kushindwa kumpa mpira KD katika sekunde za mwisho za robo ya nne ili amalize mchezo ambapo timu zote zilikuwa zimelingana pointi. Matokeo yake Green akaupoteza mpira na mechi ikaenda Over Time , Warriors wakapoteza.
Imeripotiwa kuwa ugomvi huo uliendelea mpaka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mechi kumalizika, ikisemwa kuwa Green alimtusi mara kadhaa KD kwa kumuita ‘ B**ch ‘