Beki wa Man United afuata nyayo za Zlatan Ibrahimovic
Beki wa Manchester United Victor Lindelof ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa Sweden mwaka 2018.
Beki huyo,24, anakuwa ni mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo baada ya Zlatan Ibrahimovic kuitawala tuzo hiyo kwa muda muongo mmoja.
Staa wa LA Galaxy Zlatahimovic ameshinda tuzo hiyo tangu mwaka 2007 mpaka mwaka 2016.
Mwaka 2017 akachua beki wa kati Andreas Granqvist na safari hii ameondoka nayo Lindelof.
‘ Ahsanteni sana. Ina maana kubwa kwangu kusimama hapa leo na kupokea tuzo hii, ‘ amesema Lindelof jana usiku wakati akipokea tuzo hii.
‘ Ninajivunia na ninayo furaha kubwa. Ninawashukuru wachezaji wenzangu wote, katika klabu yangu na timu ya Taifa ‘
‘ Pia ningependa kushukuru familia yangu, wamekuwa na mimi siku zote kwa mazuri na mabaya ‘
Pia mchezaji huyo alimshukuru mke wake, Maja : “ Kwa mrembo mke wangu. Ahsante sana kwa kuwepo na kuniangalia kila muda, kunisaidia na kuni-support .
Una maana kubwa sana kwangu “
Lindelof alikuwa ni moja ya nyota wa timu ya Taifa ya Sweden walioifikisha timu hiyo robo fainali ya kombe la Dunia 2018, na kutolewa na England.