Danny Welbeck afanyiwa upasuaji
Kocha wa Arsenal Unai Emery amethibitisha kuwa mshambuliaji wao Danny Welbeck amefanyiwa upasuaji kwenye kifundo chake cha mguu wake wa kulia.
Welbeck aliumia baada ya kuanguka vibaya kwenye sare ya 0-0 dhidi Sporting Lisbon kwenye mchezo wa Europa League alhamisi iliyopita.
Muingereza huyo,27, alibakia Hospitali usiku huo alioumia na kocha Emery amethibitisha kuwa amefanyiwa upasuaji siku ya ijumaa.
“ Ninafikiri hatakuwa (Welbeck) na sisi kwa muda mrefu “ alisema Emery baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Wolves hapo jana.
Welbeck sasa yupo kwenye hatihati ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu lakini kocha wake Unai Emery amekataa kuthibitisha kuwa huenda mchezaji huyo akarejea dimbani kabla ya msimu kuisha.
“ Ninafikiri ni bora kwa daktari kuongea na nyinyi.
Ni jeraha kubwa, lakini matokeo yake Daktari anaweza kujibu vizuri kuliko mimi “ amesema Unai.
Welbeck awali aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kwa ajili ya mechi za kimataifa dhidi ya USA na Croatia, lakini imeripotiwa kocha Gareth Southgate hana mpango wa kuita mbadala wake.