Benzema kwenye vitabu vya historia
Mshambuliaji wa kifaransa anayecheza soka klabu ya Real Madridi ya nchini Hispania Karim Benzema anaendeleza kupasia nyavu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2018/2019 akiichezea klabu yake ya Real Madrid.
Karim Benzema alikuwa sehemu ya timu ya Real Madrid iliyokuwa ugenini kucheza mchezo wake wanne wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Viktoria Plzen iliyokuwa nyumbani nchi ya Jamhuri ya Czech.
Real Madrid ugenini wakicheza na Viktoria wamemkung’uta kipigo takatifu cha mabao 5-0 na kuwaonesha kuwa uenyeji wao hauwezi kuwasaidia chochote mbele ya Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, magoli yakifungwa na Karim Benzema mawili dakika ya 20, 37 baada ya pasi ya Gareth Bale ambaye nae alifunga goli 40 kwa pasi ya goli kutoka kwa Benzema na akafunga tena dakika ya 93, baada ya Tony Kroos kufunga goli la nne dakika ya 67.
Ushindi huo unawaweka pazuri kwa kufikisha alama tisa sawa na AS Roma walipo nafasi ya pili, CSKA Moskva wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na alama nne na Viktoria wakishika mkia kwa kuwa na alama moja.
Kwa upande wa mfaransa Karim Benzema jina lake linaingia katika vitabu vya kumbukumbua baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo huo, yanamfanya kuingia katika vitabu vya kumbukumbu vya klabu ya Real Madrid kwa kuwa mchezaji wa saba katika historia ya klabu hiyo kufunga magoli zaidi ya 200+ Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Hugo Sanchez (208), Ferenc Puskas (242), Carlos Santillana (290), Alfredo De Stefano (208), Raul Gonzalez (323) na Cristiano Ronaldo 450 huku Benzema yeye akiwa la kafunga magoli yake yanayomfanya kufikisha 201.