Rekodi ya Harry Kane inatisha Ligi ya Mabingwa Ulaya
Mshambuliaji wa timu ya Tottenham Hotspurs Harry Kane anaendeleza jitihada zake za kudhihirisha ubora wake katika soka akiitumikia klabu yake ya Tottenham Hotspurs katika michuano mbalimbali Ulaya.
Harry Kane ambaye enzi za utoto aliwahi kuachwa na Arsenal kwa madai hakuwa na umbo la wanamichezo, kwenye usiku wa Ligi ya Mabinhwa Ulaya November 6 2018 alikuwa sehemu ya kikosi cha Tottenham kilichoingia uwanjani kupambana na PSV Endhoven ya Uholanzi katika uwanja wa Wembley.
Tottenham wakiwa ndio wenyeji wa mchezo huo wamefanikisha kuvuna alama tatu katika ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya PSV, Harry Kane akiendelea kuimarisha kitabu chake cha rekodi kwa kufunga magoli yote mawili dakika ya 78 na 89, baada ya PSV wao kupata goli mapema dakika ya 2 kupitia kwa Luuk de Jong.
Wakati ushindi huo ukiwafanya Tottenham kuvuna alama tatu na magoli mawili na kuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi lao lenye timu za Barcelona na Inter Milan, Harry Kane anaimarisha kitabu chake cha rekodi kwa kufikisha jumla ya magoli 13 na pasi mbili za usaidizi wa magoli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa kacheza michezo 13 akiwa na Tottenham wastani wa kuhusika na upatikanaji wa goli kila mechi.