Mashemeji wamemng’oa Abdulhalim Humud KMC
Uongozi wa klabu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu wa 2018/19, umetangaza kuachana na kiungo kutoka visiwani Zanzibar Abdulhalim Humoud, kufuatua kuchoshwa na matukio ya utovu wa nidhamu aliouonyesha tangu mwezi Septemba.
Katibu mkuu msaidizi wa KMC Walter Harrison Urio amethibitisha taarifa hizo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo mchana kwenye ofisi za manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Hata hivyo kabla ya kuorodhesha matukio ya utovu wa nidhamu ya mchezo huyo, Walter alianza kwa kuzungumzia mwenendo wa kikosi chao ambacho tayari kimeshashuka dimbani mara 13 kucheza michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara na kuthibitisha kuwa wameridhishwa na mwenendo huo.
Walater akaendelea kueleza mkasa mwingine wa utovu wa nidhamu uliofanywa na Abdulhalim Humoud ambao hakua tayari kuutolea ufafanuzi kutokanana sababu za kimaadili na kueleza kwa kifupi kuwa aliiba namba ya mpenzi wa mchezaji mwenzake anayeshea nae chumba wakiwa kambini na kuanza kumsumbua, Humud aliwahi kucheza Simba na Azam FC pia miaka ya nyuma.