Rooney anarudi tena kuitumikia England
Imethibitika kuwa mshambuliaji wa DC United, Wayne Rooney atarejea nyumbani kwao Uingereza kucheza mchezo wa mwisho wa kumuaga kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo.
Chama cha soka cha Uingereza FA kimethibitisha taarifa hizo na kuwa Wayne Rooney atacheza mchezo huo wa hisani kwa ajili ya kuaga maisha yake ya soka kimataifa wakati huu ambao ana umri wa miaka 33.
FA wameeleza kuwa Rooney atajumuishwa katika kikosi cha Uingereza kilichochini ya kocha Gareth Southgate ambacho kitacheza dhidi ya USA November 15, Rooney atakuwa anapata nafasi ya kucheza mchezo wake wa 120 akiwa na timu ya taifa ya Uingereza.
Mchezo huo umepewa jina la ‘’A Wayne Rooney Foundation International’ ukiwa na lengo la kutumia baadhi ya mapato kutoa msaada, kuitwa kwa Wayne Rooney katika kikosi hicho hakuwezi kuathiri idadi ya wachezaji kupunguzwa zaidi kikosi kitakuwa na wachezaji 23 na Rooney atakuwa mchezaji wa 24.
Hadi sasa Wayne Rooney ni mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Uingereza, akiwa amefunga jumla ya magoli 53 katika mechi 119 alizoichezea Uingereza na kati ya hizo wamefanikiwa kupata ushindi michezo 71, sare 29 na wamefungwa katika michezo 19 ambayo Rooney alikuwa sehemu ya timu.