Bingwa wa Kombe la Dunia ahukumiwa kwenda jela
Vincenzo Laquinta, bingwa wa kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na Italy, amehukumiwa miaka miwili kwenda jela kwa kosa la kuwa sehemu ya kundi moja la kihalifu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Juventus alifunguliwa mashitaka mwaka 2015 kwa umiliki wa silaha kinyume na sheria , na vile vile kuwa na lengo la kusaidia ‘ Ndrangheta, kundi la kimafia la linalopatikana mkoa wa Calabria, uliopo kusini mwa Italy.
Jumatano asubuhi wiki hii, Laquinta alihukumiwa jela miaka miwili kwa kukutwa na hatia ya kumiliki silaha kinyume na sheria, – bastola mbili na risasi 126 zilikutwa kwa nyumba yake huko Reggio Milia ,Italy mwezi Februari mwaka 2015.
Wakati huo huo, baba yake amekutwa na hatia ya kuwa na ushirikiano na kundi la ‘Ndrangheta ‘ na amehukumiwa jela kwa miaka 19.
Wawili hao walionesha hasira zao baada ya hukumu hizo kutoka “ Ni ujinga, aibu yenu.“ Katika familia yetu, hatujui hata ‘Ndrangheta’ ni nini, “ alisema Laquinta .
“Haiwezi kuwezekana. Wameharibu maisha yangu bila msingi, Kwa sababu ninatokea Calabria. Ninateseka kwa ajili ya familia yangu na watoto wangu. Sijafanya kitu chochote.“
Laquinta, ni mchezaji wa zamani wa klabu za Juventus, Udinese, Cesena. Alishinda kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na Italy. Pia alishinda ubingwa wa Serie A na Juventus mwaka 2013
Katika usikilizwaji wa kesi hiyo, Laquinta alieleza kuwa alinunua silaha “ kwa ajili ya siku zijazo na si kitu kingine chochote “ , kwani baada ya kuacha kucheza mpira, muda mwingi alikuwa akiutumia katika kulenga shabaha.
Hata hivyo , mchezaji huyo wa zamani hatakwenda jela mara moja kutokana na sheria za nchini Italy, mshitakiwa hatazamwi mwenye hatia mpaka pale viwango vyote vya rufaa vitakaporidhika.