Nicklas Bendtner ahukumiwa jela
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner amehukumiwa jela kwa muda wa siku 50 kwa kosa la kumshambulia dereva wa taxi.
Mdenmark huyo,30, anayecheza Norway katika klabu ya Rosenborg amekataa rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Pia mahakama imemtaka mchezaji huyo kumlipa dereva huyo pauni 1000 ( Tsh Milioni 2.9) Kama fidia.
Bendtner alivunja taya ya dereva huyo mwezi Septemba huko Copenhagen na mahakama ikaoneshwa video ya tukio hilo kutoka ndani ya taxi.
Bendtner alikataa kumlipa dereva nauli ya Pauni 4.8 ( Tsh 14,000) na baadae kuanza kumpiga,kabla ya kuendelea kumpiga akiwa amedondoka chini.
Mdenmark huyo aliomba msamaha mbele ya waandishi wa habari siku tatu baada ya tukio.
Bendtner akiomba msamaha alisema : “ Nilihusika katika tukio hili la bahati mbaya. Sikufahamu litafikia kama hivi, na ni kweli nina huzuni kubwa kwamba matokeo yake yamekuwa ya bahati mbaya kama nilivyofanya.
Kwa mashabiki na watu wote wa Rosenborg , nimejutia kilichotokea. Ninawaomba msamaha kutoka moyoni.
‘Kwa wachezaji wenzangu wote. Ninajutia kuwa hili litaleta mkanganyiko katika wakati muhimu. Ninawashukuru kwa kunielewa.’