Mourinho akataa kuzungumzia ubingwa
Kocha wa Man United Jose Mourinho amesema haoni haja ya kuongelea suala la ubingwa wakati timu yake ikiwa ipo nje ya nne bora.
United wapo nafasi ya nane pointi 9 nyuma ya vinara Man City, lakini Mourinho anasisitiza kuwa watakuwa katika nafasi ya kucheza klabu bingwa mwishoni mwa mwezi Disemba.
‘ Unapokuwa nje ya nne bora hutakiwi kuongelea mbio za ubingwa ‘ amesema Jose. ‘ Unapokuwa katika nne bora, ambapo naamini tunaenda kuwa, ndipo unaweza kuangalia juu na kuona umbali ‘
‘ Unaweza kuangalia hali ilivyo. Kwa sasa majeruhi , adhabu , kiwango……’
Tupo nje ya nne bora, kwa hiyo cha muhimu sasa ni kupata pointi tunazotaka na kufika pale mwisho wa mwezi Disemba kama ninavyotarajia. ‘
Jose Mourinho na kikosi chake kitashuka dimbani kesho kuchuana na Bournemouth ugenini.