Mourinho amtetea kocha wa Chelsea.
Chama cha soka cha England FA kimempiga faini ya pauni 6,000 ( Tsh Milioni 17) kocha msaidizi namba mbili wa Chesea Marco Ianni kwa kosa la kufanya kitendo cha kebehi kwa kocha wa Machester United Jose Mourinho baada ya goli la kusawazisha alilofunga Ross Barkley dakika za lala salama katika mechi iliyoisha kwa sare ya goli 2 – 2 Oktoba 20 Stamford Bridge.
Kocha huyu alipita mara mbili mbele ya benchi la United akishangilia kwa tambo huku akimuangalia Jose Mourinho hali iliyozua taharuki baina ya pande hizi mbili kuanzia wakufunzi hadi wachezaji.
Kitendi hicho kilimuuzi Jose Mourinho na kupelekea kuamka kwa benchi na kuanza kumfata Ianni lakini walinzi wakaingilia kati ugomvi huo.
Baada ya mechi kocha Jose Mourinho alikiri kuombwa msamaha na Maurizio Sarri pamoja Marco Ianni mwenyewe na kukiri kuupokea bila kinyongo na kusisitiza kuwa kocha huyo aachwe aendelee kufanya kazi kufuatia baadhi ya watu kupendekeza afutwe kazi.
“ Sifikiriii kuwa anatakiwa kufukuzwa. Amepita wakati mgumu lakini mwisho amegundua alikosea.
Kwangu mimi mwisho wa stori ni pale aliponiomba msamaha. Lakini ningependa kijana asipate adhabu nyingine zaidi. Muacheni afanye kazi. Kila mmoja hufanya makosa. Nimefanya makosa mengi. Ninatumaini watamuacha kijana aendelee na kazi “ Amesema kocha huyo wa Man United.