Lampard kurudi Chelsea
Chelsea wanaibuka na ushindi wa 6-1 katika uwanja wa Stamford Bridge dhidi ya Derby County, Frank Lampard akiondoka na mpira baada ya kufunga goli 4 peke yake.
Hii ndio ilikuwa ni mara ya mwisho kwa Derby County kucheza na Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge, ilikuwa ni Machi 2008.
Sasa imepita miaka 10 Derby County wanarudi katika uwanja wa Stamford Bridge, safari hii wanarudi na mtu ambaye aliwaua mara ya mwisho walipotembelea uwanja huo. Si mwingine ni Frank Lampard.
Frank Lampard anakuja na Derby County Stamford Bridge akiwa kocha mkuu wa timu hiyo.
Derby County wanacheza na Chelsea katika raundi ya 4 ya Carabao Cup.
Kuhusu kurejea kucheza dhidi ya klabu yake ya zamani aliyoitumikia kwa miaka 13 amesema kuwa ni furaha kwani ni klabu anayoipenda na pamekuwa kama nyumbani kwake.
Kukiwa na utaratibu wa wachezaji waliopo kwa mkopo timu husika kutocheza dhidi ya timu zao wanazotokea, hili litakuwa tofauti kwa siku ya leo ambapo Chelsea wametoa ruhusa kwa wachezaji wao wawili waliopo kwa mkopo Derby County Mason Mount na Fikayo Tomori kucheza mechi ya leo dhidi yao.
Hii limekuja baada ya kocha Frank Lampard kupeleka maombi kwa uongozi wa klabu yake ulioyafikisha kwa Chelsea na kupatiwa ruhusa.
Chelsea kwa upande wao wamesema itakuwa ni faida kwa wachezaji wao ambao watapata uzoefu mzuri kwa kucheza na timu kubwa za ligi kuu.
Frank Lampard na kikosi chake cha Derby County walifanikiwa kufika hatua hii baada ya kuitoa Manchester United kwa penati.
Toka atue katika timu hiyo ameifikisha katika nafasi ya mtoano kwenye Championship na sasa akiwa anahitaji kushinda hatua hii tu ili apate ifikisha timu hii hatua ya robo fainali.