Rais wa chama cha soka cha Thailand atoa heshima zake kwa mmiliki wa Leicester City baada ya ajali ya Helicopter
Rais wa chama cha soka cha Thailand FAT Soymot Poompanmoung ametoa heshima zake za mwisho kwa mmiliki wa klabu ya Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha aliyefariki katika ajali ya helikopter Jumamosi hii katika uwanja wa King Power stadium.
Tajiri huyo ni moja ya watu watano waliofariki katika ajali hiyo. Helikopta hiyo ilianguka muda kidogo tu baada ya kuruka toka uwanjani hapo lilipokuwa limemalizika pambano la Leicester City dhidi ya West Ham United waliosuluhu kwa goli 1 – 1.
Akiongea na ESPNFC Soymot alisema “Alikuwa rafiki yangu wa karibu. Inahuzunisha na tumepoteza mtu muhimu aliyefanya mengi kwa mpira wa Thiland. Ni siku ya huzuni kwa mpira wa Thai.
Vichai na kampuni yake ya King Power walioinunua Leicester mwaka 2010, walikuwa wapambe wakubwa wa Soymot alipogombea urais wa FAT kama mgombea wa mageuzi katika uchaguzi uliokuwa na ushindani February mwaka 2016.
Miezi mitatu baadae Thailand na Soymot walishangilia Leicester City kuibuka bingwa wa ligi kuu.
“Alikuwa jamaa mzuri na rafiki. Mtu aliyeweza kumsaidia yeyote aliyehitaji msaada. Alikuwa mkarimu kwa kila mtu.”
Soymot afisa mstaafu wa polisi alisema “Niliongea na Vichai juma lililopita. Tuliongelea mipango mingi ikiwa ni pamoja na kupeleka wafanyakazi toka FAT kwenda Leicester Januari ili wapate ongeza ujuzi katika nyanja za utawala, matibabu na mengine yote katika mpira.
“Tulipanga onana Bangkok Novemba 10 kwenye chakula cha jioni ili kuzungumzia mipango yote.
Alifanya mengi sana kwa mpira wa Thai na Leicester.”